Habari
MHE.MAHUNDI ATEMBELEA UBALOZI WA TANZANIA NCHINI ZAMBIA

Na Mwandishi Wetu, WHMTH, Zambia.
Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi (Mb) ametembelea ofisi za Ubalozi wa Tanzania nchini Zambia akiambatana na ujumbe wa Tanzania ulioshiriki Mkutano wa Mawaziri wa Afrika kuhusu Serikali Mtandao uliofanyika jijini Lusaka, Zambia tarehe 2 hadi 4 Oktoba, 2024.
Mhandisi Mahundi na ujumbe aliombatana nao wametembelea ofisi hizo leo tarehe 5 Oktoba, 2024 na kupokelewa na mwenyeji wake Balozi wa Tanzania nchini Zambia, Luteni Jenerali Mathew Edward Mkingule.
Ujumbe alioambatana nao ni pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru Bw. Crispin Francis Chalamila, Maafisa waandamizi kutoka Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Wizara ya Fedha, Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA), Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) na Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL).