Habari
MHE. MAHUNDI AKUTANA NA WAZIRI WA SAYANSI NA TEKNOLOJIA WA SERIKALI YA ZAMBIA

Na Mwandishi Wetu, WHMTH, Zambia
Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi (Mb) amekutana na kuzungumza na Waziri wa Sayansi na Teknolojia wa Serikali ya Zambia, Mhe. Felix Mutati tarehe 3 Oktoba, 2024.
Katika kikao hicho Mhe. Mahundi pamoja na mwenyekiti wake wamejadili masuala mbalimbali kuhusu Sekta ya Mawasiliano katika Nchi hizo mbili na kuangalia maeneo ambayo Serikali ya Tanzania inaweza kushirikiana na Serikali ya Zambia kuleta maendeleo chanya kwa Nchi zote mbili.
Mhe. Mahundi yupo Nchini Zambia kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Mawaziri wa Afrika kuhusu Serikali Mtandao (Digital Government Africa) ulio anza tarehe 2 na utamalizika tarehe 4 Oktoba 2024.