Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Habari

MHANDISI MAHUNDI AZUNGUMZA NA UJUMBE WA URUSI KUHUSU MASHIRIKIANO KATIKA SEKTA YA MAWASILIANO


Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi amekutana na kufanya mazungumzo na Ujumbe wa Serikali ya Urusi ulioongozwa na Naibu Waziri wa Mawasiliano wa Jamhuri ya Urusi Bi Bella Cherkosova, kuhusu mashirikiano baina ya nchi hizo mbili katika tasnia ya habari, mawasiliano na TEHAMA. 

Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika leo tarehe 29 Oktoba 2024 katika hoteli ya  Serena Jijini Dar es salaam, Mhandisi Mahundi ameambatana na maafisa waandamizi wa Wizara hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Dkt. Ayub Rioba, maafisa waandamizi wa. Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Tume ya TEHAMA (ICTC) na Benki Kuu ya Tanzania (BoT)