Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Habari

MHANDISI MAHUNDI AKAGUA MAENDELEO YA UJENZI WA MFUMO WA JAMII X-CHANGE


Na Mwandishi Wetu, WHMTH, Zanzibar

Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi amekagua maendeleo ya ujenzi wa mfumo wa Jamii X-Change unaounganisha mifumo ya kisekta iweze kusomana na kubadilishana taarifa ikiwa ni ufuatiliaji wa maelekezo ya Mhe. Rais Samia kwamba mifumo yote iweze kusomana na kubadilishana taarifa ifikapo mwishoni mwa  mwezi Desemba 2024.

Mhandisi Mahundi ameitembelea timu hiyo iliyokuwa katika kikao kazi cha kuwajengea uwezo wataalamu kutoka Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) kuhusu mfumo huo leo Oktoba 25, 2024 katika ofisi za Mamlaka ya Serikali Mtandao Zanzibar (eGAz).

 Pamoja na kuwapongeza wataalam hao kwa hatua nzuri waliyofikia ya kuunganisha mifumo kupitia mfumo wa Jamii X-Change, ametoa rai kwa NIDA, uhamiaji na Rita kushirikiana ili kuhakikisha watanzania wote wanapata jamii namba (namba za NIDA) zitakazopelekea kupata jamii kadi ambayo itakuwa imeunganishwa na huduma zote hivyo kuwaondolea usumbufu wa kubeba vitambulisho vingi wanapo kuwa wanahitaji huduma kutoa katika Ofisi mbalimbali.

Naye Mratibu wa Mradi wa Tanzania ya Kidijitali (DTP) Bw. Bakari Mwamgugu amesema mfumo wa Jamii X-Change unaoundwa chini ya usimamizi wa DTP umepiga hatua kubwa na mpaka sasa hivi mifumo mingi imeshaanza kusomana hivyo pasipo shaka ifikapo mwishoni mwa mwezi Desemba mwaka huu, mifumo yote ya taasisi za Serikali na zisizo za Serikali itakuwa inasomana.

Katika hatua nyingine, Mhandisi Mahundi pia ametembelea na kuona maendeleo ya ujenzi wa Mfumo wa Zan X-Change  wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) ambao unaunganisha mifumo yote ya kisekta ya Serikali ya Zanzibar