Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Habari

WATUMISHI WA WIZARA YA MAWASILIANO WAJENGEWA UWEZO KUHUSU AKILI UNDE


Na Mwandishi Wetu

Watumishi wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari wamepata fursa ya kujengewa uelewa kuhusu maendeleo na matumizi ya Akili Unde (AI) kupitia mafunzo yaliyotolewa na wadau kutoka taasisi za elimu zinazohusiana na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano.

Mafunzo hayo yamefanyika tarehe 7 Septemba 2026 katika Ofisi za Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mji wa Serikali Mtumba, Dodoma, na kufunguliwa na Mkurugenzi Msaidizi wa Uendelezaji wa Mifumo, Huduma za TEHAMA na Uzingatiaji, Mhandisi Bahati Zuberi.

Mafunzo hayo yamelenga kuongeza uelewa wa watumishi kuhusu maendeleo ya Akili Unde, matumizi yake na fursa zinazotokana na teknolojia hiyo, ili kuimarisha uwezo wa Wizara kutumia teknolojia zinazoibukia katika kuboresha utendaji na utoaji wa huduma.


#WizaraYaMawasiliano #AkiliUnde #AI #UchumiWaKidijitali #TEHAMA #DigitalTanzania #TanzaniaYaKidijitali