Habari
MAAFISA BAJETI WHMTH WAANDAA NA KUPANDISHA MPANGO WA MANUNUZI KWENYE MFUMO WA NeST

Maafisa bajeti wa kutoka katika Idara na Vitengo vya Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari wameweka kambi kazi Mkoani Morogoro kwa wiki nzima kuanzia tarehe 27 Mei 2024 kwa ajili ya kuandaa mpango wa manunuzi wa Wizara hiyo na kuupandisha katika mfumo wa manunuzi wa NeST.
Akizungumza wakati wa kikao kazi hicho, Mkurugenzi wa Kitengo cha Manunuzi cha Wizara hiyo, Bi. Kijoli Said ametoa rai kwa maafisa bajeti kuhakikisha mpango unaoandaliwa unatekelezeka ipasavyo kwa kila Idara au Kitengo kufuata taratibu wakati wa kuanzisha mchakato wa manunuzi ya bidhaa au huduma katika ofisi za umma.