Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Habari

KITUO CHA MKONGO CHA 2 AFRICA KUIFANYA TANZANIA KUWA KITOVU CHA MUUNGANISHO MAWASILIANO AFRIKA MASHARIKI NA KATI


Na Chedaiwe Msuya, Dar es Salaam.

Tanzania itakuwa kitovu cha maunganisho wa mawasiliano Afrika Mashariki na Kati kufuatia uwepo wa mkongo wa mawasiliano wa 2 Afrika utakapokamilika mwakani mwezi februari.

Hayo yameelezwa na Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt Jim Yonazi alipofanya ukaguzi wa mkongo wa kituo cha 2 Afrika Septemba 9, 2022 na kueleza kuwa hilo linafanyika kutokana na juhudi za Serikali kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha maunganisho ya mawasiliano.

Amesema kukamilika kwa ujenzi wa kituo hicho unafaida kubwa kwa nchi yetu kwa kupata mtandao wa Intaneti yenye kasi zaidi na uhakika wa kuunganishwa duniani.

“Mkongo unaokuja unapitia kusini mwa bara la Afrka, kwahiyo tutapata uhakika wa maunganisho kwenda duniani na kusaidia sana biashara ya kuuza capacity nchini mwetu nan chi Jirani na kuwasaidia wananchi wetu nan chi Jirani kuweza kushiriki katika uchumi wa kidigitali ambao ndio uchumi sasa dunia inashiriki” amesema.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Kampuni ya Airtel Tanzania, Bi. Beatrice Singano amesema wanatengeneza eneo la kusambaza mawasiliano yanayopitia baharini (Sea Cable Services) ili kuiwezesha Tanzania kufikiwa na kufikia maeneo mengine kimawasiliano.

Kituo cha Mkongo wa 2Africa Submarine kinatarajiwa kukamilika mwanzoni mwa mwaka 2023 kwa kufika katika Zaidi ya maeneo 35 katika nchi 26 Duniani.