Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Habari

Katibu Mkuu wa Mawasiliano Akutana na Ujumbe wa EU Kujadili Maendeleo ya Miradi ya Kidijitali na Ushirikiano wa TEHAMA


Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Bw. Mohammed Khamis Abdulla, amekutana na ujumbe kutoka Umoja wa Ulaya (EU) ulioongozwa na Mkuu wa Ushirikiano wa Shirika hilo, Marc Stalmans (kushoto), kujadili maendeleo ya miradi ya kidigitali ikiwemo D4T unaotarajiwa kukamilika mwezi Desemba 2026.

 

Miradi mingine ni Mradi wa Bridge Project unaosaidia utekelezaji wa Jamii Stack, na mradi wa TanTech unaotarajiwa kuanza mwaka ujao wa fedha 2026/2027 pamoja na kuimarisha ushirikiano katika sekta ya TEHAMA nchini.