Habari
Katibu Mkuu Aongoza Kikao cha Kupokea Taarifa ya Maendeleo ya Uanzishwaji wa Miundombinu Muhimu ya TEHAMA.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Bw. Mohammed Khamis Abdulla ameongoza kikao cha kupokea Taarifa kuhusu hatua zilizofikia katika Uanzishwaji wa Miundombinu Muhimu ya TEHAMA.
Kikao hiko kimefanyika leo tarehe 15 Juni, 2026 na kuhudhuriwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano, Teknolojia ya Habari na Ubunifu kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Bi Fatma Mabrouk Khamis aliyembatana na Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Maafisa Waandamizi kutoka Zanzibar.
Bw. Abdulla amesisitiza ushirikishwaji wa wataalamu wa pande zote mbili za Muungano katika kila hatua ikiwa ni pamoja na ukamilishaji wa mfumo utakaotumika kutunza Miundombinu Muhimu ya TEHAMA.
