Habari
KATIBU MKUU ABDULLA ATEMBELEA BANDA LA WIZARA 77

Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Bw. Mohammed Khamis Abdulla ametembelea banda la Wizara hiyo, lililopo katika Tenti la Jakaya Kikwete katika maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) ili kujionea jinsi watumishi wa ofisi hiyo wanavyotoa huduma kwa wananchi na wadau kwa ujumla.
Katibu Mkuu Abdulla ametembelea banda hilo tarehe 03 Julai, 2024, baada ya kushiriki uzinduzi rasmi wa maonesho hayo uliofanywa na Rais wa Jamhuri ya Msumbiji Filipe Jasinto Nyusi na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Miongoni mwa huduma alizoshuhudia Katibu Mkuu Abdulla ni pamoja na utoaji Elimu kwa Umma kuhusu Anwani za Makazi, ufafanuzi kuhusu Mfumo wa Kidigitali wa Barua za Utambulisho pamoja na Mradi wa Tanzania ya Kidigitali.
Katibu Mkuu Abdulla pia ametembelea baadhi ya Mabanda ya Taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo ambazo ni pamoja na Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN), Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC).