Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Habari

KATA 18 ZA MANISPAA YA IRINGA KUHAKIKIWA ANWANI ZA MAKAZI


Na Mwandishi Wetu, WMTH – Iringa

Kata zote 18 za Manispaa ya Iringa zimeanza zoezi la uhakiki wa taarifa za Anwani za Makazi kwa ushirikiano wa karibu kutoka kwa wataalam wa mfumo wa Anwani za Makazi kutoka Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Halmashauri ya Manispaa ya Iringa pamoja na Watendaji wa Kata.

Kata zinazoshiriki katika zoezi hilo lililoanza leo Septemba 28, 22025 ni: Kitwiru, Ruaha, Igumbilo, Mkwawa, Isakalilo, Kwakilosa, Mlandege, Mwangata, Mkimbizi, Kihesa, Mtwivila, Nduli, Gangilonga, Mshindo, Kitanzini, Ilala, Mivinjeni na Makorongoni.

Zoezi la uhakiki linatarajiwa kufanyika kwa siku 12, ambapo wataalam watafanya kazi ya kusasisha taarifa za wakazi, kurekebisha changamoto za majina ya barabara, na kuhakikisha namba za nyumba zinapangwa kwa mpangilio sahihi na unaoeleweka.