Habari
KAMATI YA BAJETI YAPOKEA TAARIFA YA MFUMO WA TTMS
Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Angellah Jasmine Mbelwa Kairuki (Mb), amewasilisha taarifa kuhusu mfumo wa kusimamia huduma za mawasiliano ya simu na intaneti uitwao Tele-Traffic Monitoring System (TTMS).
Taarifa hiyo imewasilishwa tarehe 28 Mei, 2026 mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, iliyoongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Ally Hassan Omar King, Bungeni Dodoma.
Mfumo huo ulioko chini ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) unawezesha usimamizi wa mawasiliano ya simu kwa kutoa takwimu mbalimbali zitokanazo na huduma za mitandao ya simu nchini.
