Habari
Elimu ya Mfumo wa Anwani za Makazi (NAPA) na Uombaji wa Mikopo ya Elimu ya Juu Yatolewa Dar es Salaam
Wataalam wa Mfumo wa Anwani za Makazi (NAPA) kutoka Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari wakitoa elimu kwa wananchi pamoja na wanafunzi wa Mkoa wa Dar es Salaam kuhusu matumizi ya mfumo huo pamoja na taratibu za uombaji wa mikopo ya elimu ya juu.
Zoezi hilo la siku tatu limeanza tarehe 25 Mei, 2026 kwa ushirikiano kati ya Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari pamoja na Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), likiwa na lengo la kuongeza uelewa kwa wananchi kuhusu umuhimu na matumizi ya Mfumo wa Anuani za Makazi (NAPA).
Wananchi mbalimbali pamoja na wanafunzi wamejitokeza kwa wingi katika viwanja vya Mbagala Zakhem jijini Dar es Salaam kupata elimu hiyo muhimu inayolenga kurahisisha huduma za anuani za makazi na mchakato wa uombaji wa mikopo ya elimu ya juu kupitia mfumo wa NAPA.
