Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Habari

Elimu ya maombi ya mikopo ya elimu ya juu kupitia mfumo wa NaPA yaendelea kutolewa jijini Dar es Salaam


Ikiwa ni siku ya pili ya zoezi la utoaji wa elimu kwa umma kwa wananchi kwa waombaji wa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu, wataalam wa Mfumo wa Anwani za Makazi (NAPA) kutoka Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kwa kushirikiana na Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) wameendelea kutoa elimu kwa wananchi pamoja na wanafunzi wa Mkoa wa Dar es Salaam kuhusu matumizi ya mfumo huo pamoja na taratibu za uombaji wa mikopo hiyo.

 

Zoezi hilo la siku tatu lililoanza tarehe 25 Mei, 2026 na linatarajiwa kuhitimishwa tarehe 28 Mei, 2026, likiwa na lengo la kuongeza uelewa kwa wananchi kuhusu umuhimu na matumizi ya Mfumo wa Anwani za Makazi (NAPA).

 

Wananchi mbalimbali pamoja na wanafunzi wameendelea kujitokeza kwa wingi katika viwanja vya Mbagala Zakhem jijini Dar es Salaam kupata elimu hiyo muhimu inayolenga kurahisisha huduma za anwani za makazi pamoja na mchakato wa uombaji wa mikopo ya elimu ya juu kupitia mfumo wa NAPA.