Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Habari

DKT. YONAZI AZITAKA TAASISI ZA WIZARA KUWA WABUNIFU KATIKA UTENDAJI WAO


Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt Jim Yonazi amezitaka  Taasisi za Wizara hiyo kuwa wabunifu katika kazi wanazozifanya ili kuendana na kasi ya kidijitali.

Akizungumza leo Jijini Dodoma katika kikao cha kuwasilisha Taarifa za utekelezaji wa bajeti na Majukumu ya Taasisi kwa kipindi cha julai 2022 hadi Disemba 2022 katibu Mkuu huyo Dkt Jim Yonazi  amewataka wafanyakazi hao kuongeza kasi ya ufanyaji kazi kama Mh. RaisSamia Suluhu Hassan anavyosisitiza ubunifu pamoja kushirikiana katika masuala mbalimbali.

"Kuweni wabunifu na mshirikiane kama Mh Rais samia suluhu hassan anavyosisitiza katika hotuba zake ili kuiletea nchi maendeleo katika sekta mbalimbali hapa nchini" Amesema Dkt Jim Yonazi

Aidha,Dkt Yonazi amesema kuwa nyezo pekee ni ushirikiano wa dhati katika kulitumikia Taifa na kuleta maendeleo ili kuendana na kasi ya Rais Samia Suluhu Hassan katika kuwatumikia wananchi.

Kikao cha kuwasilisha taarifa za utekelezaji wa bajeti na Majukumu ya Taasisi kwa kipindi cha julai 2022 hadi disemba 2022 kimefanyika leo Tarehe 16 February 2023 jijini Dodoma katika ukumbi wa jakaya kikwete convertion.