Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Habari

DKT. YONAZI AKUTANA NA DKT. SIMBA, JIJINI DODOMA 


Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Jim Yonazi amekutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mtendaji wa Taasisi ya Mawasiliano Afrika ya Mashariki (EACO) Dkt. Ally Simba aliyefika katika ofisi za Wizara hiyo mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma

Dkt. Simba alikuja kwa lengo la kujadiliana na Katibu Mkuu kuhusu Tanzania kuwa mwenyeji wa Mkutano wa Kwanza wa Jukwaa la Posta na Usafirishaji kwa nchi za Ukanda wa Afrika Mashariki ambao unatarajiwa kufanyika mwezi Novemba,2022 jijini ARUSHA, TANZANIA .

Vilevile katika mazungumzo yao walijadili maendeleo ya Sekta ya Mawasiliano ya Posta katika ukanda wa Afrika Mashariki hasa kwenye  nyanja za utoaji wa huduma za Mawasiliano ya Posta Kidijitali.

Waligusia kuwa kutokana na mabadiliko ya Teknolojia kugusa moja kwa moja Sekta ya Mawasiliano, hivyo Sekta ya Posta inapaswa kukabiliana na mabadiliko hayo ili kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi, na hili ndiyo lengo la kuwakutanisha watoa huduma kwenye Jukwaa moja Ili wabadilishane uzoefu.

Katika ziara hiyo Katibu Mtendaji wa EACO Dkt. Ally Simba aliambatana na Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania Bw. Macrice Mbodo.