Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Habari

MATUKIO KATIKA PICHA, DKT. BITEKO AZINDUA VITUO CHA TBC TAIFA NA BONGO FM NGORONGORO


Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Dotto Biteko (Mb) wakati akiwasili katika Uwanja wa Kassim Majaliwa uliopo Wasso-Loliondo wilayani Ngorongoro leo Aprili 15, 2024 kwa ajili ya uzinduzi wa  mradi wa usikivu wa vituo vya kurushia matangazo ya TBC Taifa na Bongo FM wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC).

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Dotto Biteko (Mb) alipokuwa akipokea maelezo kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Bi. Aisha Dachi kuhusu mradi wa usikivu wa kurushia matangazo ya TBC Taifa na Bongo FM wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) na kuzindua mradi huo leo  Aprili 15, 2024.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Aisha Dachi na Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Justina Mashiba,  wakisaini hati za makabidhiano za Mradi wa usikivu wa kurushia matangazo ya TBC Taifa na Bongo FM wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) leo  Aprili 15, 2024.

Mradi huo umezinduliwa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Dotto Biteko (Mb) ambapo amezindua mradi wa Loliondo - Ngorongoro kwa niaba ya vituo vingine ambavyo ni Makete, Kyela, Uvinza na Mbinga kwenye Uwanja wa Kassim Majaliwa.

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Dotto Biteko (Mb) akifurahia jambo na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Moses Nnauye (Mb) wakati wa hafla ya uzinduzi wa  mradi wa usikivu wa kurushia matangazo ya TBC Taifa na Bongo FM wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), leo  Aprili 15, 2024, Wasso-Loliondo wilayani Ngorongoro, mkoani Arusha.

Baadhi ya Viongozi, Watumishi na Wadau wa Mawasiliano wakiwa katika hafla ya uzinduzi wa  mradi wa usikivu wa kurushia matangazo ya TBC Taifa na Bongo FM wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), leo  Aprili 15, 2024, Wasso-Loliondo wilayani Ngorongoro.

Wananchi mbalimbali Akita katika hafla ya uzinduzi wa  mradi wa usikivu wa kurushia matangazo ya TBC Taifa na Bongo FM wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), leo  Aprili 15, 2024, Wasso-Loliondo wilayani Ngorongoro.

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Nape Moses Nnauye (Mb) akicheza ngoma ya jamii ya kimaasai na Wasonji wakati wa hafla ya uzinduzi wa  mradi wa usikivu wa kurushia matangazo ya TBC Taifa na Bongo FM wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), leo  Aprili 15, 2024, Wasso-Loliondo wilayani Ngorongoro.