Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Habari

WIZARA YAPOKEA UJUMBE WA BENKI YA DUNIA KUJADILI UTEKELEZAJI WA MRADI WA TANZANIA YA KIDIGITALI


Na Chedaiwe Msuya, WHMTH, DODOMA
 
Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari imepokea ujumbe kutoka Benki ya Dunia uliowasili kwenye Ofisi ya Wizara jijini Dodoma tarehe 29 Novemba 2022 kwa ajili ya ziara ya kutathmini utekelezaji wa Mradi wa Tanzania ya Kidigitali.
 
Ujumbe huo ambao utakuwa nchini hadi tarehe 1 Desemba 2022 uliongozwa na Dkt. Tim Kelly, ambaye ni kiongozi wa ujumbe wa Benki ya Dunia na kupokelewa na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Bw. Armon MackAchayo na Mratibu wa Mradi Bw. Honest Njau, pamoja na Menejimenti ya Wizara.
 
Baada ya mapokezi hayo, ujumbe huo ulitembelea Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora na kufanya mazungumzo na wawakilishi kutoka  Kituo cha Taifa cha Kuhifadhi Data (NIDC) na Mamlaka ya Serikali ya Mtandao (eGA) kwa lengo la kujadiliana na kutathmini utekelezaji wa sehemu ya mradi kwa upande wa eGA na NIDC.
 
Mradi wa Tanzania ya Kidigitali una thamani ya Dola za Marekani milioni 150 sawa na bilioni 349 za kitanzania na umelenga kusaidia maeneo mbalimbali katika sekta ya Habari,  Mawasiliano na TEHAMA nchini ili kufanikisha az      ma ya Serikali ya kuwa na Uchumi wa Kidijiti na kukabiliana na  mapinduzi ya teknolojia Duniani.