Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Habari

WHMTH YASHIRIKI MKUTANO WA KWANZA WA MAWAZIRI WA AFRIKA KUHUSU SERIKALI MTANDAO


Mhe. Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Injinia Kundo Andrew Mathew ameshiriki mkutano wa  “Digital Government Africa 2023” (Africa’s First Ministerial E-Government Summit) Jijini Lusaka ,Zambia. 

Katika mkutano huo, Naibu Waziri ameshiriki katika majadiliano kuhusu “Digital Government Infrastructure”. Mhe. Naibu Waziri ameelezea juu ya mafanikio ambayo Tanzania imefikia katika kuunganisha ofisi za Serikali, Halmashauri na jinsi mkongo wa Taifa ulivyounganisha nchi jirani ili kuziwezesha kupata huduma za mikongo ya baharini.

Majadiliano hayo ili washirikisha;

1. Felix Mutati- Waziri wa Sayansi na Teknolojia wa ZAMBIA
2. Ursula Owusu-Ekuful- Waziri wa Mawasiliano wa GHANA
3. Paula Ingabire- Waziri wa Tehama na ubunifu wa RWANDA
4. Haja Salimatu Bah- Waziri wa Mawasiliano, Teknolojia na Ubunifu wa SIERRA LEONE.

Kikao hiki kimefanyika leo tarehe 4 Oktoba 2023 Jijini Lusaka Zambia. Ujumbe wa Tanzania unaongozwa na Mhe. Naibu Waziri.