Habari
WAZIRI SILAA ATEMBELEA VITUO VYA UBUNIFU ARUSHA

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Jerry William Silaa (Mb.)amesema Wizara anayoiongoza ina maelekezo mahsusi ya kujenga mazingira wezeshi ya bunifu za TEHAMA, ili vijana hao waweze kujiajiri na kuchangia katika shughuli za kukuza uchumi wa nchi.
Waziri Silaa amesema hayo wakati wa ziara yake katika Chuo cha Uhasibu Arusha alipotembelea Atamizi ya bunifu mbalimbali ikiwa ni pamoja na bunifu za TEHAMA katika chuo hicho leo Machi 12, 2025.
Aidha, ameupongeza uongozi wa chuo kwa kuwa walezi wa bunifu za vijana na kuhakikisha ndoto na bunifu zao zinafikia malengo.
Ameongeza kuwa mazingira wezeshaji ya bunifu za TEHAMA yatawasaidia vijana kufanyia kazi mawazo yao na kutengeneza bidhaa zinazoweza kuingia sokoni na kuleta suluhu mbalimbali, kujitengenezea ajira na kuwezesha sekta nyingine.