Habari
WAZIRI SILAA ASHIRIKI UFUNGUZI WA MKUTANO WA KIMATAIFA WA AKILI UNDE, RWANDA

Waziri Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Jerry William Silaa (Mb) ameshiriki katika kikao cha ngazi ya mawaziri kuhusu matumizi ya Akili Unde ambacho kimefanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kigali jijini Kigali, nchini Rwanda tarehe 03 Aprili, 2025.
Kikao hicho kilichoratibiwa na Taasisi ya Tony Blair (Tony Blair Institute for Global Change - TBI) kilijikita katika kubainisha namna Akili Unde inavyoweza kutumika katika maeneo mbalimbali na kuleta ufanisi katika Sekta ya Umma barani Afrika.
Kikao hicho ni sehemu ya Mkutano wa Kimataifa wa Akili Unde Barani Afrika unaondelea nchini Rwanda kuanzia 3 hadi 4 Aprili, 2025.