Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Habari

WAZIRI SILAA AKUTANA NA RC MAKONDA, ARUSHA


Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Jerry William Silaa (Mb.), alipowasili katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha leo tarehe 12 Machi, 2025 kabla ya kuanza ziara ya siku mbili mkoani humo. 

Waziri Silaa alipokelewa na mwenyeji wake Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Paul Makonda,  na kumjulisha kuwa yuko mkoani humo kwa ajili ya kutembelea na kuzungumza na vijana wa bunifu changa za TEHAMA (Startups).

Naye Mhe. Makonda amemkaribisha Waziri Silaa na kumpongeza kwa kazi kubwa inayofanywa na wizara hususan katika eneo la mawasiliano hasa uwekaji wa minara. 

Ameongeza kuwa, ofisi yake iko tayari wakati wote kushirikiana na Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari na kwamba kuimarisha Mawasiliano kutaondosha migogoro mbalimbali katika Mkoa huo.