Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Habari

WAZIRI NAPE:KILA MWANANCHI KUPATA MAWASILIANO POPOTE ALIPO


Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye (Mb) akifanya ziara ya kukagua utekelezaji wa miradi ya mawasiliano na TEHAMA katika kijiji cha Msomera Wilayani Handeni Mkoa wa Tanga.

 

Serikali kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) imeendelea na juhudi za kufikisha huduma za mawasiliano vijijini ambapo kila mwananchi atafikiwa na huduma hiyo popote pale alipo bila kujali hali ya kiuchumi wala eneo analokaa.

 

Hayo yamebainishwa na Waziri Wa Habari,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari  Mhe. Nape Nnauye (Mb) wakati wa Ukaguzi wa hali ya mawasiliano na maabara za kompyuta katika shule ya msomera wilaya ya Handeni Mkoa wa Tanga leo machi 1 2023 ambapo amesema Kupitia mradi wa Tanzania ya Kidigitali, Serikali itafikisha huduma za mawasiliano katika maeneo mbalimbali nchini.

 

Aidha Waziri Nape amesema Serikali inaendelea na jitihada ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya mawasiliano vijijini ambapo mpaka sasa takribani minara katika kata 1,105 imekwisha washwa katika miradi ya mawasiliano katika kata 1,242.

 

“Kwa upande wa kijiji kipya cha Msomera, UCSAF kwa kushirikiana na TTCL tumetekeleza miradi ya kufikisha huduma za mawasiliano katika makazi mapya ya Msomera, Mradi huo ulitekelezwa kwa ufanisi mkubwa na Shirika la Mawasiliano TTCL ambapo kwa sasa watoa huduma mbalimbali wameweka vifaa vyao vya mawasiliano katika mnara huo.

 

“Kwa upande wa Wilaya ya Handeni, UCSAF imetekeleza miradi mbalimbali ya kufikisha huduma za mawasiliano vijijini ambapo jumla ya minara 6 imejengwa na  Watoa huduma waliofunga vifaa vyao katika mnara wa TTCL ni pamoja na Airtel, Vodacom na MIC (Tigo),”Amesema Waziri Nape.

 

Kwaupande wake  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) Peter Ulanga amesema wao kama shirika wameendelea kutekeleza maelekezo ya serikali na tayali wemekwesha kujenga kilometa 95 za faiba kutoka korogwe hadi handeni ambazo zitaongeza uwezo wakufikia kasi ya 4G.

 

Hata hivyo Mkurugenzi huyo amesema wanaendelea kuangalia usikivu wa eneo hilo kwa kushirikiana na mfuko wa mawasiliano kwa wote (UCSAF) ili kuhakikisha wanaongeza usikivu wa eneo la msomera na maeneo jirani.

 

“Sasa hivi watoa huduma wote wanapatikana hapa na tumejenga kilometa95 za faiba kutoka korogwe hadi handeni ambazo zitaongeza uwezo wakufikia kasi ya 4G na sasahivi zinatupa uwezo Zaidi ,”amesema.

 

Akizungumzia miradi hiyo Mbunge wa Handeni Vijijini Mh. John Salu amesema eneo hilo hapakuwa ya mawasiliano jambo ambalo mtu angeweza kupata matatizo asinge weza pata msada wowote.

 

Aidha ameishukuru serikali kwa kutekeleza maagizo ya Mh Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuhakikisha wanafikiwa na mawasiliano katika eneo hilo

 

“Ulikuwa ukija huku ukipata matatizo uwezi kumpigia kelele mtu yoyote kwani hakukuwa na huduma yoyote ya mawasiliano , kwakweli tu naishukuru serikali kwa kuwezesha kufikisha mawasiliano katika eneo hili,”amesema.

 

Naye Mkuu wa wilaya ya Handeni Albert Msando amesema hali ya mawasiliano katika eneo hilo ni zuri na wananchi wanaweza kupata taarifa kwa wakati kutokana na mradi huo .

 

“Wananchi wanaweza kupata huduma kutoka kwa watoa huduma wote, kwasasa hali ya mawasiliano iko vizuri siyo sehemu tena yakuchagua mtoa huduma,”amesema.