Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Habari

UFUNGUZI WA MAFUNZO YA MFUMO WA ANWANI ZA MAKAZI KWA MAAFISA TAARIFA, WENYEVITI,  WATENDAJI WA KATA NA MITAA WA HALMASHAURI YA JIJI LA DODOMA


Na, Chedaiwe Msuya, WHMTH, Dodoma.

Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini Alhaji Jabiri Shekimweri ametoa Rai kwa wanaojuhusisha na vitendo vya kung'oa nguzo za Majina ya Anwani za Makazi Katika barabara waache mara Moja vitendo hivyo kwani serikali haitosita kumchukulia hatua kali yeyote atakayebainika kufanya vitendo hivyo vyenye Nia ovu.

Kauli hiyo imetolewa leo tarehe 14 September 2023 jijini Dodoma na Mkuu wa Wilaya huyo Katika Ufunguzi wa mafunzo ya kuwajengea uwezo kuhusu Mfumo wa Anwani za Makazi Kwa Maafisa Taarifa, wenyeviti na Watendaji wa kata na Miata wa Halmashauri ya jiji la Dodoma ambapo amewataka kusimamia kwa weledi pamoja na Kutoa Elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa Anwani za Makazi.

"Kumekuwa na tabia ya baadhi ya wananchi kuharibu nguzo za majina barabara,Natoa rai kwa yeyote anayejihusisha na vitendo hivyo kuacha mara moja na sisi kama Serikali hatutasita kumchukulia hatua kali yeyote atakayebainika kufanya vitendo hivyo vyenye nia ovu". Amesisitiza

Aidha,Shekimweri amesema kuwa Anwani ya makazi ni hitaji la msingi katika kuwezesha ukuaji wa sekta mbalimbali za kijamii na kiuchumi na ni Nyenzo muhimu ya ukuaji wa uchumi wa kidijitali ambao ndio umeshika kasi katika ulimwengu wa sasa.

Sambamba na hayo Shekimweri amesema Jiji la Dodoma ni miongoni mwa miji inayokuwa kwa kasi sambambana kuwa na ongezeko kubwa la watu ambapo Takwimu za Sensa ya Watu na Makazi 2022, Jiji la Dodoma lina watu wapatao 765,179 na Kaya zipatazo 214,330.

" Hali hii inapelekea ongezeko kubwa la upimaji wa maeneo na ujenzi wa makazi mapya ambayo yanahitaji kutambuliwa na kupatiwa Anwani za Makazi pamoja na Kasi ya ukuaji wa Jiji letu inapaswa kwenda sambamba na kasi ya utambuzi na utoaji wa Anwani za Makazi". Amesema

"sisi tutakaopatiwa mafunzo tufahamu kwamba tunahitaji kwenda kuongeza kasi ya utoaji wa Anwani za Makazi". Ameongeza 

Kwa upande wake Mratibu wa wa Anwani za Makazi Bw. Jampyon Mbugi amesema Matarajio ya Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari ni kuona Jiji la Dodoma linakuwa la Mfano katika utekelezaji na matumizi ya Anwani za Makazi na kuwa chachu kwa Halmashauri nyingine kuja Dodoma kujifunza namna ya kufanikisha utekelezaji wa Mfumo wa Anwani za Makazi. 

"Na hii ndio dhamira ya Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari katika kutekeleza Mfumo wa Anwani za Makazi na Utekelezaji wa Mfumo huu ni utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) 2020-2025, Utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 na Malengo ya Dunia ya Maendeleo Endelevu hususan lengo la 8 na 9 ambayo yote kwa pamoja yanalenga kuboresha maisha ya wananchi". Amesema.

Akitoa wasilisho Kwa Maafisa Taarafa, wenyeviti na Watendaji wa kata na Miata wa Halmashauri ya Ia jiji la Dodoma, Afisa Ardhi wa Wizara ya Ardhi nyumba na maendeleo ya Makazi Anorld Mkude amesema kuwa amesama Anuani za Makazi zunamanufaa makubwa sana Katika kuiwezesha Mipango na Tafiti Kufanyika kwa Tija pamoja na Kuimarisha Ulinzi na usalama.

"Sote tunatambua kwamba suala la utekelezaji wa Anwani za Makazi ni maelekezo ya Dkt. Samia Suluhu Hassan ambayo aliyotoa siku anazindua “Operesheni Anwani za Makazi”. Maelekezo yale hayakuishia kwenye operesheni pekee bali alielekeza tuendelee kuwapatia Watanzania Anwani za Makazi ili tuweze kutambuana kwa urahisi “Nani ni Nani na Anaishi wapi”. Amesema.

Julius Magawa Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Mkoyo Kata ya Hombolo Bwawani amesema wao kama watendaji wanao wajibu wa kumsaidia kusimamia maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ili kuhakikisha dhamira yake ya dhati ya kuleta maendeleo kwa wananchi inafikiwa.

Mafunzo ya kuwajengea uwezo Maafisa Taarafa, wenyeviti na Watendaji wa kata na Miata wa Halmashauri ya Ia jiji la Dodoma kuhusu Anwani za Makazi yameandaliwa na wizara ya Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kwa Lengo la kuhakikisha kila mwananchi anatambulika kwa kutumia Anwani ya Makazi ili kuboresha mfumo wa maisha ya Watanzania na kuimarisha ufikishaji wa huduma