Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Habari

TANZANIA KUIUNGANISHA MALAWI NA MKONGO WA TAIFA WA MAWASILIANO


Na Jumaa Wange, WHMTH, Zanzibar

Shirika la Mawasiliano Tanzania-TTCL limesaini Mkataba wa Makubaliano ya Kibiashara na Kampuni ya Serikali ya Nchini Malawi inayosimamia Mkongo wa Mawasiliano - Electricity Supply Corporation of Malawi Limited (ESCOM) tarehe 08 Septemba, 2023 Kijangwani Zanzibar. 

Mkataba huo umesainiwa na Mkurugenzi waTTCL, Mhandisi Peter Ulanda pamoja Mtendaji Mkuu wa ESCOM, Bw. Kamkwamba Kumwenda na kushuhudiwa na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Nape Nnauye  (Mb) , Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Khalid S. Mohamed na  Waziri anayesimamia Mawasiliano kutoka Serikali ya Malawi (Ministry of Information and Digitalisation )Mhe. Moses Kunkuyu Kalongashawa.
 
Mkataba huo umetokana na ziara aliyoifanya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu alipofanya mapema mwaka huu nchini MALAWI.