Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Habari

DKT. YONAZI AZITAKA TAASISI NA WADAU WA BIASHARA MTANDAO NCHINI KUWA CHACHU YA UKUAJI WA HUDUMA MTANDAO


atibu Mkuu Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt. Jim Yonazi amezitaka Taasisi na wadau mbalimbali nchini wa Huduma mtandao kuwa chachu ya maendeleo ya huduma hiyo kwa lengo la kukuza uchumi nchini.

Ameeleza hayo tarehe 09 Januari, 2023, wakati akipokea taarifa rasmi ya awali ya Upembuzi Yakinifu katika Mradi wa Ujenzi wa Maghala ya kuwezesha Uhifadhi wa Bidhaa za Biashara Mtandao kutoka kwa mtaalamu mwelekezi (ALG Company).

Aidha, mradi huo unaotarajiwa kufanyika nchini ni matokeo wa utiwaji saini makubaliano ya kibiashara baina ya Posta ya Tanzania na Posta Oman uliofanyika jijini Muscat, yenye lengo la kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha biashara mtandao kwa Ukanda wa Afrika Mashariki.

Akizungumza wakati wa kikao hicho Dkt. Yonazi ametoa wito kwa Wizara na Taasisi wadau wa mradi huo kuwa kinara na chachu ya kuuwezesha mradi huu kukamilika kwa haraka zaidi ili kurahisisha biashara mtandao nchini ambapo itapelekea Tanzania kuwa kitovu cha biashara hiyo kwa ukanda wa Afrika Mashariki.

Dkt. Yonazi ameongeza kuwa uchumi wetu ni uchumi shindani na nchi nyingine. Hivyo, wadau waongeze kasi ya kukamilika kwa mradi huu kwa maendeleo ya uchumi wetu.

Dkt Jim Yonazi amesema: "Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari inaendelea kuboresha miundombinu ya Mawasiliano sambamba na Teknolojia ya Habari ili kuendelea kurahisisha upatikanaji wa huduma mbalimbali zinazoendelea kukua nchini."

Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Bi. Khadija Khamis Rajab ameeleza kuwa suala hili lina lengo la kuwaoindolea wananchi usumbufu wa kukosa uhifadhi wa bidhaa na masoko ya bidhaa zao. Aidha, alieleza uwepo wa kikao kitakachohusiana na mradi huo kwa upande wa Zanzibar na ameishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Ushirikiano unaoendelea kuwepo kwa manufaa ya pande zote mbili za Muungano