Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Habari

USIKIVU WA TBC REDIO KUIMARIKA MANYONI, SINGIDA


Na Mwandishi Wetu, WHMTH, SINGIDA

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Jerry Silaa, amesema ujenzi wa kituo cha matangazo cha TBC katika kijiji cha Mwanzi, kilichopo wilaya ya Manyoni mkoani Singida, umefikia asilimia 85 kukamilika na unatarajiwa kuboresha  usikivu wa redio za TBC na bongo FM.

Waziri Silaa alitoa taarifa hiyo baada ya kutembelea mradi huo leo Oktoba 22, 2024 wilayani Manyoni unaotarajiwa  kuanza kazi mwishoni mwa Novemba mwaka huu. 

Aliongeza kuwa Serikali inatekeleza miradi mingine kama mradi wa minara 636 nchini, ikiwemo minara 15 ya redio lengo likiwa ni kusaidia wananchi kupata habari kuhusu matukio mbalimbali nchini.

Naye Kaimu Meneja wa TBC Kanda ya Kati, Vumilia Mwasha, amefafanua kuwa mtambo huo utasaidia kuimarisha usikivu kati ya mikoa ya Dodoma na Singida