Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Habari

DKT. FAUSTINE NDUGULILE AFUNGA KIKAO CHA MAMENEJA WA TTCL MIKOA YOTE


  • TTCL Kuongeza Idadi ya Wateja kutoka Asilimia 2 hadi 6 kwa Mwaka
  • Kuongeza Idadi ya Mawakala wa Vocha, T - PESA kutoka 2,800 hadi 3,080
  • Chukueni Hatua kwa Wahujumu wa Miundombinu ya TEHAMA
  • Kuongeza Ubunifu na Utafiti wa Masoko ya Huduma na Bidhaa za TTCL
  • Boresheni Mifumo ya Huduma kwa Wateja
  • Kuingiza Mkataba na Mkurugenzi Mkuu, Mameneja Kupima Utendaji Kazi
  • Kata Huduma kwa Taasisi za Umma Zinazodaiwa na TTCL
  •  Angalieni Upya Mikataba Inayogharimu Uendeshaji wa TTCL

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndugulile amefunga kikao cha Mameneja wa Mikoa yote ya Shirika la Mawasiliano Tanzania kilichofanyika Dodoma kwa muda wa siku tatu ambacho kimehudhuriwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Zainab Chaula, Naibu Katibu Mkuu, Dkt. Jim Yonazi, Menejimenti ya Wizara na wa TTCL na wawakilishi wa taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo

 

Dkt. Ndugulile ameipongeza TTCL kwa kujiwekea malengo ya kuboresha utendaji kazi wa Shirika hilo na kuazimia kuongeza idadi ya wateja kutoka asilimia 2 hadi asilimia 6 kwa mwaka mmoja wanaotumia simu za mkononi waliopo kwenye soko; kuongeza idadi ya mawakala wa vocha na wa huduma za fedha mtandao za T – PESA kutoka 2,800 hadi 3,080 katika kipindi cha miezi mitatu; na kuboresha mifumo ya utoaji huduma kwa wateja

 

Amesema kuwa imejitokeza tabia ya baadhi ya taasisi za umma kutumia huduma za TTCL bila kulipa na amemwelekeza Mkurugenzi Mkuu wa TTCL, Waziri Kindamba kuziandikia taasisi zinazodaiwa kuwa walipe madeni yao vinginevyo ifikapo tarehe 31 Januari, 2021 wazikatie huduma hizo  

 

Ameilekeza TTCL kuchukua hatua kwa watu wanaohujumu miundombinu ya TEHAMA ya TTCL na kudhoofisha ubora wa huduma zake; kuboresha mifumo ya kuhudumia wateja ili kuongeza imani ya wateja kwa Shirika; kuangalia upya mikataba inayoigharimu Shirika ambayo imesainiwa baina ya TTCL na watoa huduma; wajiandae kuingia mikataba baina ya Wizara na Mkurugenzi Mkuu wao na Mameneja ili kupima utendaji kazi; na waongeze ubunifu na kufanya utafiti wa masoko ya huudma za bidhaa zinazotakiwa na wateja

 

Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Zainab Chaula amesema kuwa Wizara na taasisi tukipanga kwa pamoja inakuwa rahisi kuratibu, kusimamia na kufuatilia utekelezaji wa malengo na maazimio tuliyojiwekea ya kuhudumia wananchi na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo ameikumbusha TTCL kuhakikisha kuwa wanajali mazingira ya kazi ya wafanyakazi wa TTCL ili kuwaongezea ari, morali na motisha ya kuwahudumia wateja

 

Mkurugenzi Mkuu wa TTCL, Waziri Kindamba amesema kuwa wamejipanga kutekeleza maazimio na malengo waliyojiwekea ili kuomgeza huduma na bidhaa za mawasiliano kwa wananchi

 

I