Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Wasifu

Mhe. Nape Nnauye
Mhe. Nape Nnauye
Waziri

Mheshimiwa Nape Moses Nnauye ni Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari na Mbunge wa Jimbo la Mtama Mkoani Lindi. Yeye ni mwanamawasiliano na Mwanahabari mahiri wa asili ambaye anaweza kuwapa ujasiri na kuwahamasisha watu kufikia malengo ya pamoja kitaasisi. Nape ana rekodi ya mafanikio katika utumishi wa umma, akichangia majukumu na nafasi muhimu katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa tanzania na Chama Cha mapinduzi.

Alizaliwa na kukulia Tanzania. Mheshimiwa Nape Nnauye alipata Shahada ya Uzamili katika Saikolojia, Lugha na Uandishi wa Habari (Honors) kutoka Chuo Kikuu cha Bangalore nchini India, na Shahada ya Uzamili katika Utawala wa Umma kutoka Chuo Kikuu cha Mzumbe, Tanzania. Nape ni mwanataaluma mwenye bidii na ana Stashahada za Diplomasia  na Uhusiano wa Nje pamoja na ya Sayansi ya Jamii kutoka Kituo cha Uhusiano wa Nje na Chuo cha Sayansi ya Jamii cha Kivukoni, mtawalia.

Nape amehudumu kwa muda mrefu katika Chama Cha Mapinduzi (CCM), tangu siku zake za shule ya msingi. Nape alitekeleza majukumu mbalimbali ndani ya CCM na serikali, akichangia ukuaji wa kisiasa na kiuchumi nchini. Nape ni mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Kamati Kuu ya Taifa, na aliwahi kuwa Katibu wa Taifa wa Itikadi na Uenezi wa CCM.

Mhe. Nape Nnauye  ni muumini anayependa maendeleo ya Afrika na Tanzania na ameshiriki kikamilifu kutumia hazina yake ya kipekee ya maarifa na vitendo na nia na makusudi kama kijana wa Kitanzania kulijenga Taifa lake kwa uaminifu mkubwa. Mhe. Nape pia ni mshauri mwelekezi wa mawakala wa maendeleo wa baadaye wa Afrika hususani vijana wapenda maendeleo.